Wednesday, May 28, 2014

MUIGIZAJI WA KIKE RACHEL HAULE AFARIKI

MUIGIZAJI WA KIKE RACHEL HAULE AFARIKI
Muigizaji wa kike wa filamu za Tanzania (Bongo Movies) anaefahamika kwa jina la Rachel Haule amefariki leo asubuhi (May 27).

Taarifa zinaeleza kuwa muigizaji huyo alikuwa mja mzito na kwamba alijifungua kwa njia ya upasuaji (Operation) lakini kwa bahati mbaya mwanae alifariki dunia.

Imeelezwa kuwa Rachel alipelekwa katika chumba maalumu cha wagonjwa mahututi ( ICU) baada ya hali yake kuwa mbaya sana na leo asubuhi alifariki pia hivyo ni msiba wa mama na mtoto.

Watu mbalimbali wameendelea kutoa pole kwa mume wa Rachel aitwae Saguda na kuonesha jinsi walivyoguswa na msiba huo.

“Sitaki kumkufuru mwenyezi Mungu wangu! Ila kazi yake haina makosa tulimpenda ila mwenyezi Mungu kampenda zaid! inauma sana pole Saguda kwa mtihani uliokupata! Ila tupo pamoja kwa kipindi hiki kigumu.” Shilole ameandika kwenye Instagram.

No comments:

Post a Comment