Picha ya Raisi Bashar al assad.
RAIS BASHAR AL ASSAD WA SYRIA AMEKINGIA KIFUA HATUA YAKE PAMOJA NA YA JESHI LA NCHI YAKE WAKATI WA MIAKA MINNE YA MAPIGANO DHIDI YA VIKOSI VYA UPINZANI NA WANAMGAMBO WA KIISLAMU, MAPIGANO YALIZUSHA UVUMI WA KUWA ALITUMIA SILA ZA KEMIKALI KUWADHURU RAIA.
ASSAD AMESEMA KUWA WANAJESHI WAKE HAWAJASHAMBULIA SHULE WALA HAWAJATUMIA SILAHA
ZA KEMIKALI KUWAUA RAIA KATIKA KIPINDI HICHO LICHA YA MADAI CHUNGU NZIMA DHIDI
YAO.
BWANA ASAD AMEPINGA NA KUITA TUHUMA HIZO KUWA NI PROPAGANDA,
UMOJA WA MATAIFA UMEDAI
KUWA WANAJESHI WA SYRIA MARA NYINGI PIA
WALIZUIA MISAFARA YA SHIRIKA HILO KUFIKA MAENEO YA RAIA.
ASSAD AMESEMA KUWA SYRIA HAIJAWASILIANA MOJA KWA MOJA NA
MAREKANI KUHUSU VITA VYA MUUNGANO DHIDI YA KUNDI LA ISLAMIC STATE, LAKINI
AMESEMA KUWA MAREKANI ILIPITISHA HABARI HIZO
KUPITIA NCHI ZINGINE IKIWEMO IRAQ.
KATIKA MAHOJIANO NA SHIRIKA LA
HABARI LA UINGEREZA LA BBC. RAIS ASSAD AMESEMA KUWA SERIKALI YAKE ILICHUKUA HATUA YA AWALI ILI KUWALINDA RAIA NA KUPIGANA NA KILE
ALICHOKITAJA KUWA UGAIDI LAKINI HAJATUMIA KEMIKALI DHIDI YA RAIA.