Wednesday, February 11, 2015

ASSAD AKANA KUTUMIA MABOMU YA SUMU




Picha ya  Raisi Bashar al assad.

RAIS BASHAR AL ASSAD WA SYRIA AMEKINGIA KIFUA  HATUA YAKE PAMOJA NA YA JESHI LA NCHI YAKE  WAKATI WA MIAKA MINNE YA MAPIGANO DHIDI YA VIKOSI VYA UPINZANI NA WANAMGAMBO WA KIISLAMU, MAPIGANO YALIZUSHA UVUMI WA KUWA ALITUMIA SILA ZA KEMIKALI KUWADHURU RAIA.


ASSAD AMESEMA KUWA WANAJESHI WAKE  HAWAJASHAMBULIA SHULE WALA HAWAJATUMIA SILAHA ZA KEMIKALI KUWAUA RAIA KATIKA KIPINDI HICHO LICHA YA MADAI CHUNGU NZIMA DHIDI YAO.
BWANA ASAD AMEPINGA NA KUITA TUHUMA HIZO KUWA NI  PROPAGANDA,
UMOJA WA MATAIFA UMEDAI  KUWA WANAJESHI WA SYRIA MARA NYINGI PIA  WALIZUIA MISAFARA YA SHIRIKA HILO KUFIKA MAENEO YA RAIA.
ASSAD AMESEMA KUWA SYRIA HAIJAWASILIANA MOJA KWA MOJA NA MAREKANI KUHUSU VITA VYA MUUNGANO DHIDI YA KUNDI LA ISLAMIC STATE, LAKINI AMESEMA KUWA MAREKANI ILIPITISHA HABARI HIZO  KUPITIA NCHI ZINGINE IKIWEMO IRAQ.

KATIKA MAHOJIANO NA SHIRIKA LA HABARI LA UINGEREZA LA BBC. RAIS ASSAD AMESEMA KUWA SERIKALI YAKE  ILICHUKUA HATUA YA AWALI  ILI KUWALINDA RAIA NA KUPIGANA NA KILE ALICHOKITAJA KUWA UGAIDI LAKINI HAJATUMIA KEMIKALI DHIDI YA RAIA.

No comments:

Post a Comment