Picha ya KAYLA JEAN MUELLER.
RAISI WA MAREKANI BARACK OBAMA, AMETHIBITISHA TAARIFA YA KIFO CHA KAYLA JEAN MUELLER AMBAYE ALIKUWA AKISHIKILIWA MATEKA NA KUNDI LA DOLA LA KIISLAM LA SYRIA.
KAYLA RAIA WA MAREKANI KUTOKA
JIMBO LA ARIZONA MWENYE UMRI WA MIAKA 26, ALIYEKUWA AKIFANYA KAZI ZA KUTOA
MISAADA YA KIBINADAAM AMEFARIKI
WAKATI AKISHIKILIWA MATEKA NA KUNDI LA DOLA
LA KIISLAMU.
KATIKA MAELEZO YAKE RAIS OBAMA
AMESEMA,
HAIJALISHI ITACHUKUA MUDA GANI,
MAREKANI ITAHAKIKISHA HAKI INAPATIKANA KWA MAGAIDI WALIOHUSIKA KATIKA UTEKAJI
NA KIFO CHA KAYLA.
WANAMGAMBO WA KUNDI LA DOLA LA
KIISLAM, WALIDAI WIKI ILIYOPITA KUWA MATEKA KAYLA ALIUAWA KATIKA MASHAMBULIZI MAKALI YA MABOMU
YALIYOTEKELEZWA NA MAJESHI YA JORDAN KATIKA MJI WA RAQQA, WAKATI WAKILIPA
KISASI KWA KIFO CHA RUBANI RAIA WA JORDAN ALIYEUAWA NA KUNDI HILO.
KAYLA, MKAZI WA JIMBO LA
ARIZONA ALIKAMATWA NA WANAMGAMBO WA
KUNDI LA DOLA LA KJIISALM WAKATI AKITOKA HOSPITALI YA KASKAZINI MWA MJI WA
ALLEPO MWEZI AUGUST MWAKA 2013.
No comments:
Post a Comment