Monday, February 16, 2015

Mwanariadha wa mbio ndeffu Hyvon Ngetich alimaliza mita 50 za mwisho kwa kutambaa



Ingawa mwanariadha wa masafa marefu kutoka Kenya Hyvon Ngetich hakufanikiwa kushinda mbio za masafa marefu za Austin mwaka huu bila shaka alifanikiwa kuteka nyoyo za watu kutokana na ujasiri wake wa kutambaa na kuhakikisha kuwa amemaliza mbio hizo. 
Hyvon Ngetich mwenye umri wa miaka 29, aliishiwa na nguvu akiwa mita 50 kutoka kwenye mstari wa kumalizia mbio hizo na hakuweza tena kuinuka na kukimbia. Mwanariadha huyo aliamua kutambaa hadi mwisho wa mbiu hizo jambo lililowashangaza na hata kuwaliza wengi waliotazama jitihada zake. 
Muuguzi mmoja alimfuata kwa karibu mkimbiaji huyo akiwa tayari kumsaidia iwapo angeishiwa kabisa. Muuguzi huyo hata hivyo hakumgusa wala kumpatia msaada wowote Ngetich jambo ambalo lingesababisha jitihada zake kukataliwa.
Akiongea kuhusu jambo hili la kushangaza Mkurugenzi wa mashindano hayo ya Austin, John Conley alisema kuwa hajawahi kuona jambo kama hilo katika miaka 43 aliyohusika na mbio za masafa marefu. 
John Conley aliyezungumza na Ngetich baada ya kumaliza mbio hizo alimwambia kuwa alikuwa ameonyesha ujasiri mkubwa katika kukimbia na kutambaa kwake. Conley aliahidi kumpa Ngetich tuzo sawa na mshindi wa nafasi ya pili licha ya kumaliza wa 3 kwani alikuwa katika nafasi ya 2 alipoanza kutambaa. 
Ngetich alimaliza katika nafasi ya 3 kwa muda wa 3:04:02, nyuma ya mshindi wa mashindano hayo Cynthia Jerop kutoka Kenya vile vile aliyemaliza kwa muda wa 2:54:21 na Mmarekani Hannah Steffan aliyemaliza wa 2 kwa muda wa 3:03:69.

Wednesday, February 11, 2015

ASSAD AKANA KUTUMIA MABOMU YA SUMU




Picha ya  Raisi Bashar al assad.

RAIS BASHAR AL ASSAD WA SYRIA AMEKINGIA KIFUA  HATUA YAKE PAMOJA NA YA JESHI LA NCHI YAKE  WAKATI WA MIAKA MINNE YA MAPIGANO DHIDI YA VIKOSI VYA UPINZANI NA WANAMGAMBO WA KIISLAMU, MAPIGANO YALIZUSHA UVUMI WA KUWA ALITUMIA SILA ZA KEMIKALI KUWADHURU RAIA.


ASSAD AMESEMA KUWA WANAJESHI WAKE  HAWAJASHAMBULIA SHULE WALA HAWAJATUMIA SILAHA ZA KEMIKALI KUWAUA RAIA KATIKA KIPINDI HICHO LICHA YA MADAI CHUNGU NZIMA DHIDI YAO.
BWANA ASAD AMEPINGA NA KUITA TUHUMA HIZO KUWA NI  PROPAGANDA,
UMOJA WA MATAIFA UMEDAI  KUWA WANAJESHI WA SYRIA MARA NYINGI PIA  WALIZUIA MISAFARA YA SHIRIKA HILO KUFIKA MAENEO YA RAIA.
ASSAD AMESEMA KUWA SYRIA HAIJAWASILIANA MOJA KWA MOJA NA MAREKANI KUHUSU VITA VYA MUUNGANO DHIDI YA KUNDI LA ISLAMIC STATE, LAKINI AMESEMA KUWA MAREKANI ILIPITISHA HABARI HIZO  KUPITIA NCHI ZINGINE IKIWEMO IRAQ.

KATIKA MAHOJIANO NA SHIRIKA LA HABARI LA UINGEREZA LA BBC. RAIS ASSAD AMESEMA KUWA SERIKALI YAKE  ILICHUKUA HATUA YA AWALI  ILI KUWALINDA RAIA NA KUPIGANA NA KILE ALICHOKITAJA KUWA UGAIDI LAKINI HAJATUMIA KEMIKALI DHIDI YA RAIA.

KARDINALI KARL JOSEPH BECKER AMEFARIKI DUNIA

Picha ya  KARDINALI KARL JOSEPH BECKER


 BABA MTAKATIFU FRANCISKO AMEPOKEA TAARIFA YA MSIBA WA KARDINALI KARL JOSEPH BECKER KUTOKA SHIRIKA LA WAYESUIT, ALIYEFARIKI DUNIA, TAREHE 10 FEBRUARI 2015 KWA MAJONZI MAKUBWA NA AMEMTUMIA SALAM ZA RAMBI RAMBI MHESHIMIWA PADRE ADOLFO NICOLÀS PACHON, MKUU WA SHIRIKA LA WAYESUIT, KWA KUMKUMBUKA KARDINALI BECKER KWA SADAKA NA MAJITOLEO YAKE KATIKA MAISHA NA UTUME WA KANISA.

NI KIONGOZI ALIJIPAMBANUA KWA KUWAFUNDA VIJANA WA KIZAZI KIPYA, HUSUSAN MAPADRE KATIKA TAFITI ZA KITAALIMUNGU PAMOJA NA HUDUMA KWA KANISA LA KIULIMWENGU. BABA MTAKATIFU ANAMWOMBA BIKIRA MARIA NA KWA MAOMBEZI YA MTAKATIFU INYASI WA LOYOLA, WAWEZE KUMWOMBEA MAREHEMU KARDINALI BECKER, ILI AWEZE KUPOKELEWA KATIKA MAISHA YA UZIMA WA MILELE.

KARDINALI BECKER ALIZALIWA KUNAKO MWAKA 1928, NCHINI UJERUMANI, AKAJIUNGA NA SHIRIKA LA WAYESUIT AKIWA NA UMRI WA MIAKA ISHIRINI. BAADA YA MASOMO NA MAJIUNDO YAKE YA KIKASISI, AKADRISHWA KUNAKO MWAKA 1958. KWA MIAKA MINGI AMEKUWA NI JAALIM LA MAFUNDISHO TANZU YA KANISA, HUKO FRANKFURT NA KATIKA CHUO KIKUU CHA KIPAPA CHA GREGORIAN, KILICHOKO MJINI ROMA. ALIKUWA NI MJUMBE WA BARAZA LA KIPAPA LA MAFUNDISHO TANZU YA KANISA. KUNAKO TAREHE 18 FEBRUARI 2012 ALITEULIWA NA BABA MTAKATIFU MSTAAFU BENEDIKTO XVI KUWA KARDINALI, AMEFARIKI DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 86.

KARDINALI PIETRO PAROLIN, KATIBU MKUU WA VATICAN ANAUNGANA NA WOTE WANAOOMBOLEZA KIFO CHA KARDINALI BECKER, ALIYEPENDWA NA KUHESHIMIWA SANA NA VIJANA WA KIZAZI KIPYA, KUTOKANA NA HEKIMA NA UMAHIRI WAKE KATIKA KUFUNDISHA; ANAMWOMBEA MAISHA YA UZIMA WA MILELE. 

KIFO CHA KAYLA



Picha ya KAYLA JEAN MUELLER.
RAISI WA MAREKANI BARACK OBAMA, AMETHIBITISHA TAARIFA YA KIFO CHA KAYLA JEAN MUELLER AMBAYE ALIKUWA AKISHIKILIWA MATEKA NA KUNDI LA DOLA LA KIISLAM LA SYRIA.

KAYLA RAIA WA MAREKANI KUTOKA JIMBO LA ARIZONA MWENYE UMRI WA MIAKA 26, ALIYEKUWA AKIFANYA KAZI ZA KUTOA MISAADA YA KIBINADAAM  AMEFARIKI WAKATI  AKISHIKILIWA MATEKA NA KUNDI LA DOLA LA KIISLAMU.

KATIKA MAELEZO YAKE RAIS OBAMA AMESEMA,
HAIJALISHI ITACHUKUA MUDA GANI, MAREKANI ITAHAKIKISHA HAKI INAPATIKANA KWA MAGAIDI WALIOHUSIKA KATIKA UTEKAJI NA KIFO CHA KAYLA.

WANAMGAMBO WA KUNDI LA DOLA LA KIISLAM, WALIDAI WIKI ILIYOPITA KUWA MATEKA KAYLA  ALIUAWA KATIKA MASHAMBULIZI MAKALI YA MABOMU YALIYOTEKELEZWA NA MAJESHI YA JORDAN KATIKA MJI WA RAQQA, WAKATI WAKILIPA KISASI KWA KIFO CHA RUBANI RAIA WA JORDAN ALIYEUAWA NA KUNDI HILO.

KAYLA, MKAZI WA JIMBO LA ARIZONA  ALIKAMATWA NA WANAMGAMBO WA KUNDI LA DOLA LA KJIISALM WAKATI AKITOKA HOSPITALI YA KASKAZINI MWA MJI WA ALLEPO MWEZI AUGUST MWAKA 2013.

Tuesday, February 10, 2015

Sifa za raisi ajae za tajwa na Mh Shamsi Vuai Nahodha

 Mh. Shamsi Vuai Nahodha.
Kutaja sifa za mgombea kunahitaji hekma kubwa sana kwani watu wanaangalia sura,hali ya mgombea na mambo mengine. Lakini ni tofauti na matarajio ya wengi pale wanapomchagua mtu wa namna hiyo.
  
  Mh shamsi Vuai Nahodha ametaja sifa za mgombea kupitia matatizo ya wananchi wa Tanzania "ukita kutaja sifa za mtu unae taka akumtumikie kwanza angalia masharti na matakwa yako"
            MATATIZO YA WA TANZANIA
             1. Nitaifa changa
             2. Utegemezi
             3. Muungano
             4. Mmomonyoko wa maadili
          hayo ni mambo yanayo wasumbua watanzania kutokana na Mh Nahodha. kutokana na hayo akataja sifa za kiongozi ambae ataweza kuitumikia nchi ya Tanzania kuwa ni Mwadilifu, Mtendaji na mwenye dhamira ya kujenga taifa la kujitegemea.

Nikki Wa Pili- Safari

Monday, February 2, 2015

Diamond atu mjini songea kumpa nguvu raisi

Baada ya kuwa kigoma kwaajili ya kufanya ngoma yake na Linex. Msanii wa kizazi kipya Nasibu Abdul pamoja na penzi jipya lake Zali waungana na wana ccm kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa chama hicho. Diamond alifanya show katika uwanja wa majimaji ulio katikati ya mji wa songea.